Chagua app inayofaa biashara yako. Tunajenga mifumo ya kisasa kwa kila aina ya biashara nchini Tanzania.
Fanya mauzo hata bila internet! Sakinisha kwenye kompyuta yako (Windows 10/11) — POS kamili, stoki, risiti na ripoti zinazofanya kazi offline. Internet inahitajika mara moja tu kusajili duka.
Hatua 5 rahisi (maelekezo kamili yapo ndani ya ZIP)
Inayopatikana sasa + zinazokuja karibuni.
Mfumo Kamili wa POS kwa Wafanyabiashara
Mfumo wa Point of Sale (POS) ulioundwa mahsusi kwa maduka ya vifaa vya shule na ofisi nchini Tanzania.
POS kwa saluni za kunyoa & urembo
MAUZO BARBERSHOP ni mfumo wa kisasa wa kuuza (POS) uliotengenezwa maalum kwa vinyozi, saluni za kunyoa na vituo vya urembo. Unakuwezesha kuuza huduma (kunyoa, kusuka, kuchonga ndevu) na bidhaa (shampoo, mafuta, vifaa); kupokea malipo ya Taslimu, Mobile Money, Kadi na Deni; kufuatilia mapato ya kila kinyozi (commission); kutunza taarifa za wateja; na kupata ripoti za mauzo. Unapatikana kwa Kiswahili na Kiingereza.
MFUMO WA MATOKEO
Achana na Excel na kujaza matokeo kwa mikono! Pakia alama za wanafunzi, mfumo utakokotoa jumla, wastani, madaraja na nafasi wenyewe. Tengeneza ripoti, andaa ratiba, na tuma matokeo kwa wazazi kwa SMS — yote mahali pamoja.
POS kwa migahawa & hoteli
Mfumo wa POS uliotengenezwa maalum kwa migahawa, cafe, na hoteli. Mizani ya meza, menyu, oda za jikoni, na bili.
POS kwa famasi & maduka ya dawa
Tarehe za kuisha kwa dawa, batch numbers, na ripoti za TFDA.
POS kwa maduka ya jumla & grocery
Barcode scanner, kategoria nyingi, na promosheni.
POS kwa maduka ya nguo & fashion
Saizi, rangi, mitindo, picha za bidhaa, na ufuatiliaji wa stoki kwa variants.
Apps zetu zote zina encryption ya hali ya juu.
Mawasiliano yote kwa Kiswahili.
Pata updates mpya bila malipo ya ziada.
Tuko hapa kukusaidia kuchagua app inayofaa biashara yako.